Monthly Archives: December 2018

SHUTMA ZA UJASUSI MTANDANO DHIDI YA UCHINAKWA UFUPI: Australia, Marekani na Uingereza zimeitupia lawana nchi ya Uchina kuhusika na ujasusi mtandao katika mataifa yao na mataifa Rafiki – Shutma ambazo zime eleza uchina kuhusika na wizi wa taarifa za siri za kibiashara za serikali na makampuni ya Teknologia.
---------------------------
Niliwahi kueleza mara kadhaa mwelekeo mpya na hatari wa Uhalifu mtandao ambapo nilitahadharisha kuhusiana na vita mtandao (Cyber Warfare) pamoja na Ujasusi Mtandao (Cyber Espionage) ambavyo kwa sasa mataifa makubwa yanawekeza zaidi kwenye matumizi ya teknolojia kudhuru na kuingilia mataifa mengine kimtandao.

Kundi la APT-10 la uchina limeshutumiwa na Uingereza na Marekani kuingilia makampuni takriban 45 ya Teknolojia, Taarifa za wafanyakazi takriban laki moja za wanajeshi wa majini wa marekani pamoja na computer mbali mbali za shirika la NASA.Zhu Hua pamoja na Zhang Shilong, ambao ni raia wa Uchina wameshtakiwa na Marekani kuhusika na kufanya mashambulizi mtandao kwaniaba ya wizara ya ulinzi ya uchina (Chinese Ministry of State Security) – Naibu Mwanashria mkuu wa Marekani , Bwana  Rod Rosenstein alielezea shutma hizo.


Uchina imekana kuhusika na shutma zinazotolewa dhidi yake na marekani pamoja na uingereza huku ikiitaka marekani kuwaachia raia wake wawili – Shutma ambazo  zimeelezwa athari zake zimekumba nchi nyingine takriban 12 ikiwemo Nchi ya Brazil, Japan, Ufaransa, Canada na Nyinginezo.

Aidha, Kumekua na shutma mfano wa hizi kutokea taifa moje dhidi ya Jingine ambapo Mataifa kama Urusi, Korea ya Kaskazini, Marekani, Uingereza, na Uchina zimekua zikitwajwa zaidi kua na tabia ya ujasusi mtandao – Huku ikionekana mataifa hayo yakiongeza nguvu na kujiimarisha kua na uwezo mkumbwa wa kufanya mashambulizi mtandao kwa mataifa mengine.Sanjari na hili, tumeona ukuaji mkubwa makampuni kutoa huduma za kiuhalifu mtandao kama vile “Malware – as –a service”, “Ransomware – as – a service” na “Cyberattacks on demand” jambo ambalo limepelekea uhalifu mtandao kuendelea kushika kasi maeneo mengi duniani.

Hivi karibuni, Shirika la Kipelelezi la marekani (FBI) limefungia makampuni kadhaa yanayo jihusisha na huduma za kutoa msaada wa mashambulizi mtandao kwa wateja wake.

FBI, imeeleza makampuni yaliyo fungiwa yamekua yakijihusisha na huduma za kushambulia mashirika ya kifedha, Mashule, wakala wa serikali, watoa huduma za kimtandao nakadhalika.

critical-boot.com, ragebooter.com, downthem.org, and quantumstress.net ni baadhi tu ya waliokumbana na zilzala ya funga funga iliyofanywa na shirika la kipelezi la marekani (FBI) baada ya oparesheni kubwa kufanyika dhidi ya makampuni yanayo jihusisha na huduma za kihalifu mtandao.Aidha, Katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka takwimu zimekua zikionyesha uhalifu mtandao unakua kwa kasi, na tumekua tukishuhudia matukio mengi ya kihalifu mtandao yanayopelekea upetevu mkubwa wa pesa na taafifa za watu binafsi pamoja na makampuni mbali mbali.

Nikitokea mfano kwa mataifa yetu ya Afrika mashariki, Nchini Kenya kwa mujibu wa takwimu zilizo tolewa na “Communications Authority of Kenya (CA)”, imeelezwa kubainika matukio ya kihalifu mtandao zaidi ya Milioni 3.8 kwa kipindi cha miezi mitatu pekee. Taarifa za Kina Juu ya hili zimechapishwa na "STANDARD MEDIA" ya Kenya.

Nitumie Fursa hii, Kushauri umakini zaidi wakati wa kutumia mitandao hususan huduma za kibenki za kimtandao na kuimarisha zaidi ulinzi wa mifumo yetu ya kimtandao ili kupunguza ukubwa wa tatizo.