AHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA KWA KOSA LA KUHARIBU TAARIFA ZA ALIYEKUA MUAJIRI WAKE


KWA UFUPI: Steffan Needham, Amabae alihudumu kama mshauri wa maswala ya tehama (IT Cosultant) katika kampuni ya Voova ya nchini Uingereza amehukumiwa kifungo cha miaka 2 Jela kwa kosa la kuharibu taarifa za muajiri wake wa wa zamani.
——————————–

Kwa mujibu wa Thames Valley Police ya Nchini Uingereza, Mtuhumiwa alifukuzwa kazi na mwaajiri wake na baadae kuharibu taarifa zote muhimu za kampuni hiyo kwa kile kilicho tafsiriwa kama kulipiza kisasi kutokana na kufukuzwa kwake.
Uharibifu wa taarifa umekadiriwa kuigharimu kampuni hiyo kiasi cha Dola laki sita na elsfu Hamsini (US$650,000) ikiwa ni pamoja na kupelekea wafanyakazi kadhaa kupoteza kazi zao.

Mtuhumiwa amehukumiwa chini ya sheria ya nchini Uingereza ya mitandao (Computer Misuse Act)Aidha, Kampuni husika imeonekana na mapungufu ya kushindwa kuwa na mikakati madhubuti ya kulinda taarifa zake ikiwa ni pamoja na uwekaji wa njia zaidi ya moja (multi-factor authentication) ya uthibitishaji pale mhusika anapotaka kuingia kwenye mifumio yake na kuhakiki ufutwaji wa taarifa katika mfumo unahusisha mtu zaidi ya mmoja.

Ushauri umetolewa kwa makampuni kuchukua tahadhari za dhati katika kulinda taarifa zake ili kujikinga na watumishi wasio wema walio ndani (Malicious/disgruntled insiders) kuweza kuleta maafa hapo baadae.


Wakati huo huo, mahakama Nchini marekani imepatia kibali cha ruhusa kwa Microsoft kuziangusha tovuti takriban 99 zilizo husishwa na uhalifu rubunishi (Phishing Attack).

Tom Burt, kutokea Microsoft ameeleza oparesheni iliyo ziharibu na kuziangusha tovuti hizo 99 ilihusisha makampuni mengine makubwa kama vile Yahoo na mengineyo.